Kutengeneza Mtandao imara, wenye nguvu na ushawishi ili kuwaleta pamoja vijana na wanawake katika kujenga mtazamo chanya juu ya Mustakabali wao (Mapinduzi ya kifikra) na kuhakikisha mgao sawa wa rasilimali katika maendeleo ya nchi uwe ni haki ya kila raia
Kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujitolea ili kuigusa jamii yenye uhitaji ili kutengeneza na kukuza mazingira ya usawa kwa jamii.
01Kukuza ubunifu na vipaji kibiashara kwa vijana na wanawake ili kuwa kuwafungulia fursa za kujiajiri.
02Kujenga uchumi wezeshi na jumuishi kupitia miradi bunifu na ujasiriamali ambayo itawainua na kuongeza hamu au kuchochea jitihada za maendeleo..
03Kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali tutaendesha tafiti zinazohusu mambo ya vijana na wanawake ili kujenga ufahamu, ubobevu na kuviarifu vyombo vya maamuzi juu ya sera za vijana na wanawake
04Kuanzisha na kujenga mtandao imara wa vijana ambao utakuwa ndio sauti, ushirikishwaji, uwezeshaji wa rasilimali kwa shughuli mbalimbali za vijana
05Kushirikishana katika ubunifu, uvumbuzi na uwezeshaji katika kuleta mapinduzi na kukuza matumizi sahihi ya kidigitali.
06Taifa Letu, Kesho Yetu Movement ni mtandao wa vijana uliopo nchi nzima ambapo unaoendesha vuguvugu la kujitolea ili kuleta mapinduzi ya kifikra katika jamii na unaamini kuwa mgao sawa wa rasilimali za Taifa letu ni haki ya kila raia.
Mtandao huu unaunganisha vijana na kuhimiza ushiriki wao wa moja kwa moja katika fursa mbalimbali ili kuharakisha maenedeleo nchini kote katika sekta za kiuchumi, kijamii, kidijitali na kitamaduni bila kujali dini, itikadi za kisiasa, kabila au ukanda.
Kujenga mtandao imara wenye lengo la kuleta mapinduzi ya kifikra kwa vijana na wanawake.
Jiunge sasaKutengeneza Mtandao imara, wenye nguvu na ushawishi ili kuwaleta pamoja vijana na wanawake katika kujenga mtazamo chanya juu ya Mustakabali wao (Mapinduzi ya kifikra) na kuhakikisha mgao sawa wa rasilimali katika maendeleo ya nchi uwe ni haki ya kila raia.
Jiunge sasaUtaifa, Uzalendo, Usawa, uwezeshaji, ubunifu, ushirikiano na ujumuishi.
Jiunge sasaMtandao huu unaunga mkono falsafa za 4R za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa yaani Ustahimilivu, Kujenga upya Taifa, Upatatisho wa Taifa na Marekebisho.
TK Movement ni Mtandao unaopinga kikundi au taasisi yoyote ile inayogawa Taifa misingi ya udini, Ukabila, Ukanda au kupandikiza chuki kwa Watanzania ili kuchukia mamlaka halali za Serikali.
Mtandao huu unaojengwa kwa misingi ya Kujitolea, Utaifa na uzalendo utaendelea kulinda na kuenzi tunu za Taifa.
Mtandao huu unayalinda na kuyaenzi Mapinduzi matukufu Zanzibar ya Januari, 12 mwaka 1964.
Mtandao huu utaendelea kulinda na kuenzi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kupingana na Vikundi vyote vinavyotaka kudhoofisha Muungano wetu.